Baada ya muigizaji na mchekeshaji kutokea Tanzania Idris Sultan kupata nafasi ya kushiriki kwenye movie mpya ya “The Blue Maritius” inayotarajiwa kuanza kutengenezwa March, 2018 itakayogharimu dola milioni 20 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 40 ikichezwa katika nchi mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini, Berlin, London, Paris, Acapulco na Mexico.
Idadi ya waigizaji watakaoshiriki kwenye movie hiyo inazidi kuongezeka baada ya muigizaji kutokea kwenye filamu maarufu ya ‘Captain America’ Anthony Mackie kupata mchongo huo na kukamilisha timu ya waigizaji 9 watakaoshiriki kwenye movie hiyo wakiwemo waigizaji kama Pearl Thusi, John Rys, Ernest Napoleon na Eric Dane.
ANOTHER GREAT HOLLYWOOD ACTOR TO BE IN THE SAME MOVIE WITH IDRIS SULTAN
Reviewed by loy
on
October 13, 2017
Rating:
No comments: